Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Tazara Mbeya kilianzishwa Mwaka 1992 kikiwa na Wanachama waanzilishi 123 na Mtaji wa Tshs 600,000/=. Kilipata Usajiri rasmi 20.10.1994.
Nambari ya kuandikishwa ni MBR 349. Hadi sasa chama kina Jumla ya Wanachama 1300 ambapo Wanaume ni 1000 na Wanawake 275 na Vikundi vya Wajasiriamali 25.
Idadi ya Wanachama imeendeleo kuongezeka siku hadi siku pia Wateja wanaofungua akaunti za Amana (Current Account) wamefikia 2000. Akaunti za Amana zinazofunguliwa katika Chama chetu hazina Makato ya kila Mwezi hivyo huwasaidia sana Wajasiliamali Wadogo, Vikundi/Vikoba, Wafanyakazi na Wananchi kwa Ujumla.
Chama kina Jumla ya Mtaji wa Tshs 4.5 Bilioni ikiwa Hisa za Wanachama ni zimefikia thamani ya Tshs 680 Milioni na Akiba na Amana za Wanachama ni Tshs 3.8 Bilioni.